Jose Mourinho
Meneja wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuwa na msururu wa matokeo mabaya.
The
Blues walishinda Ligi ya 'Premier' msimu uliopita lakini msimu huu
mambo yamekuwa kinyume, na wamo pointi moja tu juu ya eneo la kushushwa
daraja ligini.
Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich.
Mreno huyo mwenye umri wa miaka 52 amekuwa Chelsea kwa kipindi cha pili, kilichoanza Juni 2013.
Chelsea
walimaliza alama nane mbele kileleni msimu uliopita na kutwaa taji
pamoja na Kombe la Ligi lakini mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa
mechi tisa kati ya 16 ligini kufikia sasa.
Mechi ya mwisho kwa Mourinho kwenye usukani ilikuwa Jumatatu walipochapwa na viongozi wa ligi Leicester City 2-1.
Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos na miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi.
BBC
Hakuna maoni :