SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KAMUSOKO AIPAISHA YANGA KILELENI DAKIKA ZA USIKU.





YANGA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga jioni ya leo.

Bao hilo pekee la mabingwa hao watetezi lilifungwa na kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe, Thabani Scara Kamusoko katika dakika ya 95 na kuwarejesha wana Jangwani hao kileleni.



Kamusoko alifunga bao hilo kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya kichwa ya Mzimbabwe mwenzake, Donald Dombo Ngoma ambaye naye alipokea krosi ya winga Godfrey Mwashiuya.

Yanga SC inafikisha pointi 26, baada ya kucheza mechi 11, ikiizidi pointi moja Azam FC yenye mechi moja mkononi, ambayo sasa inachukia nafasi ya pili.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Malimi Busungu, Donald Ngoma na Deus Kaseke/ Godfrey Mwashiuya.
African Sports; Ramadhani Mwaluko, Mwaita Ngereza, Khalfan Twenye, Juma Shemvuni, Rahim Juma, Mussa Chambega/Ally Ramadhani ‘Kagawa’,
Mussa Kizenga/James Mendi, Pera Ramadhani, Hassan Materema, Mohammed Mtindi/Hussein Issa na Mohamed Issa.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply