SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / NDOTO KUTIMIA-MBWANA SAMATTA NJIANI ULAYA JANUARI, KUTUA KRC GENK!


SAMATTA-TZSTRAIKA MAHIRI wa Tanzania anaechezea Klabu ya Congo DR, TP Mazembe Mbwana Samatta yuko njiani kwenda Ulaya kujiunga na Klabu kubwa ya Belgium KRC Genk.

Kwa mujibu wa Jarida la kuaminika la France, L’Equipe, TP Mazembe na Genk wamefikia makubaliano kwa Fowadi huyo hatari kuhamia Genk Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho likifunguliwa.

Inaaminika Samatta atasaini Mkataba wa Miaka Minne na Nusu na Genk ambayo inacheza Ligi Kuu ya Belgium iitwayo Belgian Jupiler League na wao wapo Nafasi ya 6 baada ya Kushinda Mechi 8, Sare 4 na Kufungwa 8 Msimu huu.

Msimu huu, Samatta amewika mno Afrika akiwa na TP Mazembe kwa kufunga Bao 8 kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI na kuwapa Ubingwa wao wa 5 wa Afrika.

HABARI ZA NYUMA:

MBWANA SAMATTA ATINGA 3 BORA YA MCHEZAJI BORA AFRIKA!

STRAIKA MAHIRI wa Tanzanian Mbwana Ally Samatta ametinga kwenye 3 Bora ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka kwa wale wachezao ndani ya Afrika.

Samatta, anaechezea Klabu Bingwa ya Afrika TP Mazembe ya Congo DR, alifunga Bao 7 kwa Mazembe zikiwemo Bao 2 wakati wa Fainali ya kutwaa Ubingwa wa Afrika.


Wachezaji wengine Wawili watakauchuana na Samatta kuwania Tuzo hii ni Mchezaji mwenzake wa TP Mazembe, Kipa Robert Kidiaba na Mchezaji kutoka Algeria anaechezea Etoile Du Sahel, Baghdad Boundjah.

3 Bora ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka wale Mapr
ofeshenali wan je itagombewa na Andre Ayew (Ghana/Swansea City), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon/Borussia Dortmund) na Yaya Toure (Cote d"Ivoire/Manchester City)

Washindi wa Tuzo hizi, ambao hupatikana kwa Kura za Makocha Wakuu au Wakuu wa Ufundi wa Vyama Wanachama wa CAF, watatangazwa Januari 7 kwenye Hafla maalum iitwayo Glo-CAF Awards Gala.

Mchezaji Bora Afrika wa Mwaka
Andre Ayew (Ghana/Swansea)
Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon/ Borussia Dortmund)
Yaya Toure (Cote d"Ivoire/ Manchester City).
Mchezaji Bora Afrika wa Mwaka – wanaocheza ndani ya Afrika
Baghdad Boundjah (Algeria/: Etoile du Sahel)
Mbwana Ally Samata (Tanzania/ TP Mazembe)
Robert Kidiaba (DR Congo/ TP Mazembe) ‎
Mchezaji Bora Afrika wa Mwaka - Kinamama
Gabrielle Onguéné, Cameroon
Gaelle Enganamouit, Cameroon
Ngozi Ebere, Nigeria
N'rehy Tia Ines, Cote d’Ivoire
Portia Boakye, Ghana
Mchezaji Bora Kijana Afrika wa Mwaka
Adama Traore, Mali
Kelechi Nwakali, Nigeria
Samuel Diarra, Mali
Victor Osimhen, Nigeria
Yaw Yeboah, Ghana
Kipaji kinacholeta matumaini       
Azubuike Okechukwu, Nigeria
Etebo Oghenekaro, Nigeria
Djigui Diarra, Mali
Mahmoud Abdelmonem ‘kahraba’, Egypt
Zinedine Ferhat, Algeria
Kocha wa Mwaka  
Baye Ba, Mali, U17
Emmanuel Amunike, Nigeria U17
Fawzi Benzarti, Etoile Sportive de Sahel
Hervé Renard, Cote d’ivore
Patrice Carteron, TP Mazembe
Refa wa Mwaka
Alioum, Cameroon
Bakary Papa GASSAMA, Gambia
Eric Arnaud OTOGO CASTANE, Gabon
Ghead Zaglol GRISHA, Egypt
Janny SIKAZWE, Zambia
Lejendari wa Mwaka
Charles Kumi Gyamfi, Ghana
Samuel Mbappé Léppé, Cameroon
Timu ya Taifa Bora ya Mwaka
Cote d’Ivoire
Ghana
Mali U17
Nigeria U17
Nigeria  U-23
Timu ya Taifa Bora ya Mwaka - Kinamama
Ghana
Cameroon
South Africa
Zimbabwe
Klabu ya Mwaka
USM Algers, Algeria
TP Mazembe, DR Congo
Orlando Pirates, South Africa
Etoile Sportive du Sahel, Tunisia

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply