Rais wa
Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amewapa siku saba
kuanzia tarehe 03/12/2015 wafanyabiashara wote ambao waliingiza mizigo
yao bila kulipa kodi wakalipe kwani baada ya hapo watachukuliwa hatua
kali za kisheria
Hayo yamesemwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam na Mheshimiwa Rais katika mkutano wake na wadau wa sekta binafsi alipoamua kufanya mazungumzo nao pamoja na kuwasikiliza maoni yao ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika kipindi cha kampeni za kuomba kura za kiti cha Urais,lengo likiwa ni kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta binafsi.
Mheshimiwa Rais aliendelea kusema kuwa katika kipindi hichi cha miaka mitano amedhamiria kuijenga nchi na watu wasimuelewe vibaya kwa maamuzi anayofanya kwani ni kwania njema ya kuleta maendeleo na siyo ujeuri.
“Tutaangalia namna ya kupunguza utitiri wa ushuru katika bidhaa mbalimbali,mfano katika kipindi cha kampeni niligundua katika Mkoa wa Kagera na Kilimanjaro wanakolima zao la Kahawa,wamekuwa wakitozwa tozo 26 kwa zao hilo na hiyo imechangia kusababisha wafanyabiashara wa zao hilo kufanya biashara haramu ya kupeleka zao hilo kwa magendo kuuza katika nchi jirani”,alisema Mheshiwa Rais Dkt. Magufuli.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Dkt.Magufuli amewaahidi wadau wasekta binafsi ushirikiano mkubwa kwani anatambua mchango wao katika kukuza uchumi na pia amewataka wadau hao kuwa wazalendo na kuliacha kukwepa kulipa kodi ili tuweze kujenga taifa lenye maendeleo makubwa ya kiuchumi.
Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli ameendelea kusema kuwa kama kutakuwa na mfayabiashara yeyote atakayetaka kuwekeza na akakwamishwa na mtu aliyechini ya uteuzi wake basi mtu huyo ataondoka kwani sasa ni wakati wa wadau wa sekta binafsi kuanza kuanzisha viwanda mbalimbali vitakavyo toa ajira.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli amewapa mawazo ya kibiashara wadau wa sekta binafsi kuanzisha kampuni ya kutenganisha udongo unaotoka kwenye machimbo ya madini,kuanzisha viwanda vya samaki pembezoni mwa bahari pamoja na kutengeneza samani zitokanazo na mazao ya misitu.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw.Regnald Mengi amesema kuwa wako tayari kumpa ushirikiano mkubwa Mheshimiwa Rais katika kuhakikisha uchumi watanzania unakuwa kwa haraka na pia amemuomba mheshimiwa rais kuendelea kukemea masuala ya rushwa pamoja kusaidia kupunguza utitiri wa kodi

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Reginald Mengi akiongea katika mkutano huo na kumuahidi Rais Dkt. Magufuli ushirikiano katika kutekeleza yale anayodhamiria kwenye serikali yake ikiwemo kusimamia ulipaji kodi kwa dhumuni la kuiinua Tanzania kiuchumi
Baadhi ya
Wadau wa Sekta Binafsi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano huo Ikulu leo Jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Reginald Mengi akimpongeza Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipomaliza
kutoa hotuba kwa wajumbe wa Sekta Binafsi nchini Ikulu leo Jijini Dar es
Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza
Jambo Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Reginald Mengi
wakati wa Mkutano na Wadau wa Sekta Binafsi nchini Ikulu leo Jijini Dar
es Salaam.
Picha na Hassan Silayo
Picha na Hassan Silayo
Hakuna maoni :