SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / TASWIRA YA SAMATTA NA ULIMWENGU WAKIWA NDANI YA SUTI ZA TP MAZEMBE, VIPI YANGA NA SIMBA?



Yanga na Simba ndiyo wakongwe katika soka la nyumbani na huenda wanapaswa kuwa mfano katika mambo mengi sana.

Lakini mambo yanavyokwenda wamekuwa wakichelewa na kuwa wa mwisho katika mambo mengi sana pia.
Suala la wachezaji kuwa katika mwonekano mzuri wanapokuwa wanasafiri, inaonekana kama hilo litafanyika lazima wavae ‘traksuit’.
Hivi kwani wao hawawezi kuvaa angalau suti na kuwa katika mwonekano bomba kabisa. Mfano angalia picha hiyo ya vijana wawili nyota Watanzania.
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, hawa wawili wanakipiga katika klabu ya TP Mazembe. Picha hiyo inawaonyesha wakiwa nchini Japan walikokwenda kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa klabu.
Lazima tukubali, kupitia mengi tunaweza kujifunza kupitia Ulimwengu na Samatta. Vijana wetu, wadogo zetu, ndugu zetu hawa lakini juhudi zao zinafanya watupe somo kubwa na lazima tuziheshimu na kuzithamini.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply