Kwa
wanaofatilia siasa za kenya kulikua na skendo iliyokua inamuhusu waziri
wa uhuru Anne Waiguru, huyu Anne Waiguru alikua ni waziri mtu mkubwa na
maarufu serikalini.
Zimepotea
795 milion kshs ambazo ni kama 16 billion tz shs amewajibishwa na
nyumbani kwake kumepekuliwa na maofisa wa kupambana na rushwa na kukuta
mamilioni ya pesa kwenye mabunda, soon atafunguliwa mashtaka na
kufungwa.
Juzi
hapa Tanzania ufisadi wa escrow umetu cost zaidi 300 billions lakini
hakuna hata mmoja aliyepekuliwa na wote wamerudi kua wabunge.
Tunatakiwa
kuiga wakenya, sio tunatimua maofisa wa tra na muhimbili alafu tunaanza
kujiisifu sana bado tuna safari ndefu kwenye hii vita dhidi ya ufisadi.
Sina nia ya kubeza anachofanya Magufuli, nampongeza ila tunapaswa kushinikiza yafanyike zaidi ya hapa na tumuunge mkono.
Kenya wana upinzani imara ndio maana kukitokea ubadhirifu kidogo tu wanaibana serikali hadi inawachukulia hatua wahusika.
Tusiwabeze
wapinzani wa serikali tuwasapoti maana wao ndio wanaweza kuibana
serikali kwa niaba yetu panapofanyika madudu kama haya
Hakuna maoni :