KLABU ya Yanga imekiri kuwa haitaweza kumsajili
mshambuliaji wa Stand United na timu ya taifa ya Tanzania Elias Maguli,
kutokana na mkataba mpya aliosaini kwenye timu hiyo hivi .
“Tumeuangalia na kujiridhisha kwamba haitawezekana kumsajili Maguli kipindi hiki cha dirisha dogo kutokana na garama kubwa ya pesa ambayo tutatumia katika kuvunja mkataba wake hivyo tutaendelea kutumia washambuliaji tuliokuwa nao au kama tukipata mchezaji mwingine wa nafasi hiyo na kocha akiridhishwa naye tunaweza kumchukua vinginevyo hatutasajili mchezaji kipindi hiki,” amesema Tiboroha.
Maguli ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi ya Vodacom akifunga mabao tisa kwenye mechi 10 alizoichezea timu hiyo na tangu kufunguliwa kwa dirisha la usajili timu nyingi zimeonyesha kupigana vikumbo kuwania saini yake ikiwemo TP Mazembe ya DR Congo, Yanga na Azam FC.
Yanga walianza kummezea mate Maguli baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwa hivi karibuni akiwa na klabu yake pamoja na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilipocheza na Algeria na kufunga bao la kwanza katikasare ya 2-2 nyumbani.
Hakuna maoni :