Simba imejiongezea ppointi tatu za Ligi Kuu Bara baada ya kuitwanga Ndanda FC kwa bao 1-0.
Licha
ya Simba kuchezesha wachezaji wote saba katika kikosi cha kwanza
wanaotokea katika mataifa matano ya kigeni, shujaa wao ameibuka kuwa
Ibrahim Ajib aliyefunga bao pekee katika dakika ya 81.
Kama
utajumlisha wachezaji hao kutokea katika mataifa matano ya kigeni yaani
Ivory Coast, Kenya, Zimbabwe, Uganda na Burundi pamoja na Tanzania,
maana yake Simba ilichezesha wachezaji kutoka mataifa sita tofauti
katika wachezaji 11 walioanza katika kikosi cha kwanza.
Ushindi
huo ulikuwa mgumu kwa Simba ambayo ililazimika kufanya kazi ya ziada
kutokana na kutocheza kwa kiwango cha juu sana huku Ndanda wakitoa
upinzani mkali.
Anagalau baada ya kupatikana kwa bao hilo, Simba walizidi kuiandama Ndanda wakitaka kupata bao la pili, lakini haikuwezekana.
Kocha
Dylan Kerr alipanga kikosi chenye wachezaji wote saba wa kigeni ambao
wanaruhusiwa na Shirikisho la Soka Tanzania na kufanya aweke rekodi mpya
ya kikosi kuanza na wachezaji wote wageni.
Wageni
walioanza katika kikosi cha leo cha Simba ni Vicent Agban (Ivory
Coast), Emiry Nimuboma (Burundi), Justice Majabvi (Zimbabwe), Paul
Kiongera (Kenya) na Hamisi Kiiza, Brian Majwega (wote Uganda).
KIKOSI KAMILI CHA SIMBA KILICHOANZA LEO
KIKOSI KAMILI CHA SIMBA KILICHOANZA LEO
1. Vicent Agban
2. Emiry Nimuboma
3. Mohammed Hussein 'Tshabalala'
4. Juko Murshid
5. Abdi Banda
6. Justice Majabvi
7. Danny Lyanga
8. Mwinyi Kazimoto
9. Hamisi Kiiza
10. Paul Kiongera
11. Brian Majwega
Hakuna maoni :