NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora,
Suleiman Jafo, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauli ya Manispaa
ya Ilemela, John Wanga kutokana matumizi mabaya ya madaraka.
Waziri Jafo amefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa ufujaji wa
fedha za ujenzi wa uzio wa halmashauli hiyo ulioghalimu Sh. 347 milioni
pamoja na kukaidi kuhamia kwenye nyumba ya Serikali ya Sh. 200 milioni.
Naibu huyo wa Tamisemi alitoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi
wa manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ambako amesema mkurugenzi huyo
ameshindwa kuhamia katika nyumba hiyo ambayo inakadiliwa kughalimu Sh.
200 milioni na kusababisha Serikali kuendelea kulipia nyumba anayoishi.
Amesema kuwa licha ya Serikali kutoa agizo mkurugenzi huyo kuhamia
katika nyumba hiyo lakini yeye aliendelea kupangishia nyumba nzima
inayolipiwa Sh. 2 milioni kwa mwezi licha ya kukamilika kwa nyumba
iliyojengwa.
Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe CCM amesema kuwa katika manispaa
hiyo kuna matatizo mengi na kwamba itatumwa kikosi cha uchunguzi kutoka
Tamisemi ili kufanya uchunguzi namna ambavyo fedha za ujenzi wa uzio
zilivyotumika ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa watakaobainika kuhusika
na suala hilo.
“Huu ukuta (uzio) hauwezi kughalimu fedha zote hizo, nyie hata kwa madai
yenu mnayosema mlifanya haraka kwa sababu ya uchaguzi sio kweli
hamtaweza kushawishi kwa hilo.
“Watanzania wana shida, dawa hospitalini hakuna, wakina mama
wanajifungulia chini halafu, milioni 200 imekaa tu haina shughuli yeyote
ile, mkurugenzi unapaswa kupisha uchunguzi kufanyika kwanza,” amesema
Jafo.
Hata hivyo amesema kuwa ujenzi wa nyumba hiyo ulianza tangu mwaka 2013
lakini mpaka sasa mkurugenzi huyo amekataa kwenda kuishi kwa sababu ya
kuwa chini ya kiwango na kwamba ipo katika maeneo hatarishi.
Amesema licha ya uongozi wa manispaa hiyo kujipangia kiwango cha Sh. 2
milioni kwa mwezi,kiwango hicho kipo juu ya kiwango cha serikali cha
laki nane.
Kwa upande wake mkurugenzi, Wanga katika kujitetea amesema sababu
zilizosababisha kushindwa kuhamia katika nyumba hiyo ni kutokana na kuwa
katika eneo hatarishi ikilinganishwa na nafasi yake ya ukurugenzi.
“Waziri (Naibu Waziri Tamisemi) tunafanya kazi kubwa za wananchi na kazi
zetu mnazifahamu tunafanya watu wengine hawapendi tunachokifanya, sasa
nikihamia katika nyumba ile na ukilinganisha na eneo ilipo ni hatari,”
amesema Wanga.
Home
/
MATUKIO
/
Breaking News: Naibu Waziri -Tamisemi Seleman Jaffo Amsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza
Breaking News: Naibu Waziri -Tamisemi Seleman Jaffo Amsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :