Bao la
Mtibwa Sugar walilofunga katika dk 10 za mwisho za mechi yao dhidi ya
Mtibwa Sugar katika michuano ya Mapinduzi, ndiyo gumzo zaidi katika
mitandao leo.
Bao
Hilo lilifungwa na Ramadhani Kichuya na mwamuzi msaidizi akainua
kibendera kuonyesha mfungaji kabla aliotea, ingawa mazingira yote
yalipingana na mwamuzi huyo.
Kutokana
na hali hiyo, mashabiki wa soka wamekuwa wakilijadili bao hilo, wengi
wakionekana kupinga kwamba kuna walakini lakini wako wanaoamini mwamuzi
alikuwa sahihi.
Mjadala umekuwa mpana zaidi katika makundi mengi ya wapenda soka, wakibishana na kujadiliana kwamba kipi ni sahihi au si sahihi.
Mechi
hiyo iliisha kwa sare ya bao 1-1 huku Mtibwa Sugar ikionyesha soka safi
na la kuvutia ingawa ilishindwa kuibuka na ushindi.
Hakuna maoni :