SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / FA CUP: IJUMAA LIVERPOOL KUANZA NA EXETER, JUMAMOSI MECHI KEDEKEDE.

FACUP-ARSENAL15-FBFA CUP, ambalo sasa linaitwa Emirates FA Cup kwa sababu za kiudhamini na ni Kombe kongwe kabisa Duniani, litaanza kurindima Ijumaa Usiku huko England kwa Mechi pekee huko Mjini Exeter kati ya Exeter City FC na Liverpool.

Huu ni mwanzo wa Mechi za Raundi ya 3 FA CUP, inayoshirikisha jumla ya Timu 64, ambayo Klabu za Ligi Kuu England na Daraja la chini yake, The Championship, huanzia kampeni zao na nyingine hufuzu toka Raundi zake za awali kabisa.

Exeter City, Timu ya Ligi 2, ambayo ni Daraja la 4 kwa Mfumo wa England, wamefanikiwa kutinga Raundi ya 3 na sasa ni Wenyeji wa Klabu kigogo Liverpool.

Raundi hii ya 3 imeibua Mechi 5 za Timu za Ligi Kuu England kuvaana wenyewe kwa wenyewe na moja ya hizo ni ile Mechi tamu huko White Hart Lane ambako Tottenham watawavaa ‘Maajabu’ ya Ligi Kuu England Leicester City ambao wako Nafasi ya Pili katika Msimamo wa Ligi hiyo.

Arsenal, ambao ndio Mabingwa Watetezi baada ya kulitwaa Kombe hili kwa mara ya pili mfululizo Mwezi Mei Mwaka huu, Jumamosi watakuwa kwao Emirates kucheza na Sunderland wakati Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, Chelsea, Jumapili wapo kwao Stamford Bridge kucheza na Timu ya Daraja la chini Scunthorpe United.

Siku ya Jumamosi Manchester United wapo kwao Old Trafford kucheza na Sheffield United wakati Man City wako Ugenini kucheza na Norwich City.
FA CUP
Raundi ya 3
***Saa za Bongo
Ijumaa Januari 8
2255 Exeter v Liverpool    
Jumamosi Januari 9
1545 Wycombe v Aston Villa       
[Mechi kuanza Saa 12 Jioni]
Arsenal v Sunderland                 
Birmingham v Bournemouth                 
Brentford v Walsall           
Bury v Bradford               
Colchester v Charlton                 
Doncaster v Stoke            
Eastleigh v Bolton            
Everton v Dag & Red                 
Hartlepool v Derby           
Huddersfield v Reading              
Hull v Brighton                
Ipswich v Portsmouth                
Leeds v Rotherham          
Middlesbrough v Burnley            
Newport v Blackburn                  
Northampton v MK Dons            
Norwich v Man City          
Nottm Forest v QPR
Peterborough v Preston              
Sheff Wednesday v Fulham                  
Southampton v Crystal Palace               
Watford v Newcastle                  
West Brom v Bristol City             
West Ham v Wolves         
2030 Man United v Sheffield United                
Jumapili Januari 10
1500 Oxford United v Swansea             
1700 Carlisle v Yeovil                 
1700 Chelsea v Scunthorpe                  
1900 Tottenham v Leicester                 
2100 Cardiff v Shrewsbury          


THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3
Ijumaa 9 Januari 2016
Raundi ya 4
Jumamosi 30 Januari 2016
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali
Jumamosi 12 Machi 2016
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali
Jumamosi 21 Mei 2016

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply