SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / FA CUP: MABINGWA WATETEZI ARSENAL WATOKA NYUMA NA KUSHINDA, CITY NAO SAFI.

FACUP-ARSENAL-SUNDERLANDMABINGWA WATETEZI wa FA CUP, ambalo sasa huitwa EMIRATES FA CUP kwa sababu za kiudhamini, Arsenal, Leo wameanza kampeni ya utetezi wao kwa kutoka nyuma na kuifunga Sunderland Bao 3-1 Uwanjani Emirates Jijini London.

Sunderland walianza kufunga kwa Bao la Dakika ya 17 la Jeremiah Lens na Arsenal kusawazisha katika Dakika ya 25 kwa Bao la Joel Campbell.

Bao hizo zilidumu hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili, Arsenal waliongeza Bao 2 katika Dakika za 72 na 75 za Aaron Ramsey na Olivier Giroud.

Nao Man City, wakicheza Ugenini huko Carrow Road, waliichapa Norwich City Bao 3-0 kwa Bao za Sergio Aguero, Dakika ya 16, Kelechi Iheanacho kufunga Dakika ya 31 na Kevin De Bruyne Dakika ya 78.

VIKOSI:
Arsenal: Cech, Bellerin, Gabriel, Koscielny, Gibbs, Chambers, Oxlade-Chamberlain, Campbell, Iwobi, Walcott, Giroud
Akiba: Arteta, Ramsey, Monreal, Macey, Reine-Adelaide, Willock, Debuchy.

Sunderland: Pickford, Yedlin, Coates, O’Shea, Van Aanholt, Lens, Toivonen, Cattermole, Watmore, Fletcher, Graham
Akiba: Jones, Borini, Defoe, M’Vila, Mannone, Beadling, Mavrias.
Referee: Martin Atkinson

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply