RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli
huenda akasafiri kwa mara ya kwanza nnje ya nchi toka aingie madarakani
mwishoni mwa mwaka jana kuelekea nchini Ethiopia ambapo atakutana na
viongozi wa serikali na Nchi za Afrika zaidi ya 50 katika kikao cha 26
cha Mkutano wa Umoja wa Afrika Mjini Addis Ababa, Ethiopia baadaye wiki
hii.Masuala ya amani na ulinzi yatakuwa katika ajenda ya juu hasa
ikichukuliwa kile kinachoendelea katika nchi ya Burundi na pia
mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika nchi za Burkina Faso na
Somalia.
Viongozi wa serikali na nchi za Afrika wanatazamiwa
kushiriki katika kongamano la 26 la Baraza Kuu la Umoja wa Afrika,
litakalofanyika kati ya Januari 30 na 31 ambapo pia watamchagua
Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Nchi za Afrika(AU).Kwa mara nyingine tena
viongozi wa Umoja wa Afrika(AU) wanatazamiwa kushinikiza kufanyika
mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Licha ya pingamizi
kutoka nchi 5 wanachama wa kudumu wa baraza hilo huko nyuma, viongozi wa
AU wamesema kwa mara nyingine tena watashinikiza mageuzi katika chombo
hicho, wakisisitiza kuwa muundo wa sasa wa baraza hilo hauakisi hali
halisi ya siasa na uchumi wa dunia katika karne hii ya 21.Kamati ya nchi
10 za Kiafrika juma lililopita ilifanya kikao na kuafikiana kuwa
maslahi ya nchi Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndio
miongoni mwa ajenda kuu za kikao cha Addis Ababa.
Nchi hizo ni Algeria,
Libya, Senegal, Sierra Leone, Namibia, Zambia, Uganda, Kenya,
Equatorial Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Viongozi hao
wanatazamiwa kurejea mwito wao wa kutaka nchi mbili za Kiafrika ziwe
wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa sasa
nchi 5 wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN ni Marekani,
China, Russia, Ufaransa na Uingereza.Viongozi wa Kiafrika wanazituhumu
nchi wanachama wa baraza hilo kuwa hazina demokrasia na kwamba zimekuwa
zikitumia kura zao za veto kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Viongozi wa
Umoja wa Afrika aidha wanapendekeza kuongezwa idadi ya nchi wanachama wa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoka 20 hadi 25.
Hii itakuwa ni
nafasi kwa Rais Magufuli kufanya safari ya nje ya nchi kwa mara ya
kwanza tokea achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania.Rais magufuli kwa sasa
amekuwa gumzo katika majukwaa ya kimataifa kutokana na aina ya uongozi
wake ambao wachambuzi wa kisiasa wanadai ni nadra kuupata kwa viongozi
wan chi za Afrika ambapo rushwa, ufisadi, uvivu na ubadhirifu wa mali ya
umma ni moja ya maisha ya viongozi wakuu wa nchi.
Hakuna maoni :