SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / HIVI NDIVYO WAZIRI NAPE ALIVYOMPA SAMATTA BONGE LA SAPOTI


Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa, Nape Nnauye leo ameungana na Mwanasoka Bora Afrika, Mbwana Samatta na Watanzania wapenda soka na michezo kumpongeza.

Nape ametumia karibu siku yake yote kuwa na Samatta ambaye ameshinda tuzo hiyo na kuweka rekodi mpya nchini na barani Afrika.

Kama unakumbuka, kabla ya Samatta kuondoka kwenda Nigeria kwenye fainali ya tuzo hizo, alikwenda ofisini kwa Nape kumuaga na kuchukua baraka zake.

"Mtoto ni vizuri ukapata baraka za wazazi, nimeona nije hapa kwa mheshimiwa waziri kumuaga na kuchota baraka zake," alisema siku hiyo Samatta.

Waziri Nape naye kama alimtabiria baada ya kumueleza kwamba Serikali inamuunga mkono kwa wakati wote na ana imani atafanya vizuri na kurejea na tuzo hiyo ambayo kweli amerejea nayo.




«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply