LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumamosi Januari 16
1545 Tottenham v Sunderland
1800 Bournemouth v Norwich
1800 Chelsea v Everton
1800 Man City v Crystal Palace
1800 Newcastle v West Ham
1800 Southampton v West Brom
2030 Aston Villa v Leicester
+++++++++++++++
JUMAMOSI Manchester City na Leicester City zina nafasi murua ya kutwaa uongozi wa Ligi Kuu England ikiwa watafanya vyema kwenye Mechi zao na kwa vile Vinara Arsenal wao wanacheza Jumapili.
Arsenal na Leicester City zote zipa Pointi 43 lakini Arsenal wako juu kwa ubora wa Magoli wakati Man City wako Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 40.
Hiyo Jumamosi, Man City, ambao Jumatano walitoka 0-0 na Everton, wako kwao Etihad kucheza na Crystal Palace na Leicester City, waloiachapa Tottenham 1-0 Siku ya Jumatano, wako Ugenini Villa Park kucheza na Aston Villa.
Sare au ushindi kwa Leicester utawaweka Leicester kileleni lakini wakifungwa na City kushinda basi City watatwaa uongozi pengine hadi Jumapili ambapo ushindi kwa Arsenal, wakiwa Ugenini dhidi ya Timu ngumu Stoke City, utawarejeshea Arsenal uongozi wao wa Ligi.
Katika Mechi yao ya mwisho huko Anfield, Arsenal walitoka 3-3 na Liverpool.
Mbali ya Mechi hii ya Arsenal, Jumapili pia ipo Bigi Mechi ya Mahasimu wakuu huko England kati ya Liverpool na Man United, Klabu ambazo zina Masapota wengi huko na pia zenye mafanikio makubwa kupita zozote Nchini humo.
Kama ilivyo kwa Sare ya Liverpool ya 3-3, Man United nao walitoka 3-3 na Newcastle huko Saint James Park Siku ya Jumane
.
Kimsimamo, Man United wako Nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 34 na Liverpool ni wa 9 wakiwa na Pointi 31.
Katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu iliyochezwa huko Old Trafford, Man United waliitwanga Liverpool 3-1 hapo Septemba 12 kwa Bao za Blind, Herera [Penati] na Martial, ambae alikuwa akicheza Mechi yake ya kwanza kabisa, wakati lile la Liverpool lilifungwa na Benteke.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumapili Januari 17
1705 Liverpool v Man United
1915 Stoke v Arsenal
Jumatatu Januari 18
2300 Swansea v Watford
Hakuna maoni :