KEPTENI
wa Manchester United, Wayne Rooney, ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa
Mwaka kwa 2015 akitetea tena Tuzo ambayo pia aliizoa 2014.
Hii ni mara ya 4 kwa Rooney kuzoa Tuzo hii ambayo Wachaguaji wake ni Masapota wa Timu ya Taifa ya England.
Mapema Desemba England ilianika Listi ya Wagombea wa Tuzo ya
Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Nchi yao ambapo pia ipo Tuzo kwa Chipukizi
Vijana wa chini wa Miaka 21, U-21.
Kepteni wa England, Wayne Rooney, ambae alishinda Tuzo hiyo Mwaka Jana, ni miongoni mwa Wachezaji Watano waliokuwa wakiigombea.
Rooney Mwaka 2015 aliiongoza England kufuzu kuingia Fainali za
Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, ambazo zitachezwa huko France Mwezi Juni
huku akihakikisha England inashinda Mechi zao zote 10 za Kundi lao na
kuifungia Jumla ya Bao 5 kwa Mwaka 2015 kwa England huku pia akiivunja
Rekodi ya Sir Bobby Charlton ya Ufungaji Bora katika Historia ya England
kwa kufunga Bao 50 Rekodi ambayo iliwekwa na Charlton Mwaka 1968
alipofunga Bao lake la 49.
++++++++++++++++++++++++++++++++++
Wagombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka:
Joe Hart (Manchester City)
Gary Cahill (Chelsea)
Raheem Sterling (Manchester City)
Wayne Rooney (Manchester United)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)
++++++++++++++++++++++++++++++++++
Kwa Vijana wa U-21, Listi ya Wagombea Watano nayo ilianikwa.
++++++++++++++++++++++++++++++++++
Wagombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa U-21:
Jack Butland (Stoke City)
Carl Jenkinson (West Ham United)
James Ward-Prowse (Southampton)
Jesse Lingard (Manchester United)
Nathan Redmond (Norwich City)
++++++++++++++++++++++++++++++++++
Kura kwa Wagombea hawa zilipigwa Mtandaoni na Masapota wa England na upigaji ulifungwa Jumapili Januari 3.
Rooney alijizolea Kura Asilimia 37, Harry Kane 30% na Hart 19%.
Kwa upande wa Vijana U-21 Kipa wa Stoke Jack Butland ndie Mshindi.
Hakuna maoni :