WAZIRI wa Katiba na Sheria,Dk.Harrison Mwakyembe amesema kuwa suala la
kuanzisha mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi wanafanyia kazi na
muda sio mrefu watatoa taarifa juu ya hatua walizofikia.
Dk.Mwakyembe ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Ofisi ya Mkurugenzi
wa Mashitaka nchini (DPP),amesema kuwa suala mahakama linafanyiwa kazi
kwa karibu na ofisi yake kutokana na ahadi ya Rais Dk.John Pombe
Magufuli wakati wa kampeni.
Mwakyembe amesema kuwa watu ambao wanaweza kuleta maendeleo ya nchi ni
vyombo vilivyo katika maamuzi ya kisheria hivyo lazima viweze kufanya
kazi kwa wananchi kwa kutenda haki.
Amesema kuwa baadhi ya watendaji wa taaluma ya sheria sio waaminifu kwa
kujihusisha na rushwa na kufanya watendaji wote kuharibika kwa sababu ya
mtu mmoja.
Mwakyembe amesema yeye ni mwanasheria na kuongeza kuwa kuna’
majipu’katika tasnia ya taaluma ya sheria na kuwataka majipu hayo
yatumbuliwe kabla ya Rais Dk.John Pombe Magufuli hajayatumbua bila
sindano ya kupunguza maumivu (Ganzi).
Mwakyembe amesema kuwa wanajua changamoto ya mawakili wa serikali
wanazokumbana nazo ikiwemo miundombinu pamoja na mfumo wa maisha
wanayoishi hivyo serikali itafanya uwezeshaji kadri ya uwezo wao.
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini,Buswello Mganga amesema katika mafanikio
walioyapata ni pamoja kushinda kesi nane za dawa za kulevya kwa
watuhumiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 30.
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :