VIGOGO
wa Jiji la Madrid huko Spain, Real Madrid na Atletico Madrid, Jana wote
walitoka Sare kwenye La Liga na kuwaacha Mabingwa Watetezi Barcelona
wapete kileleni huku wakiwa na Mechi 1 mkononi.
Juzi Barca waliichapa Malaga 2-1 na kutwaa uongozi wa La Liga huku wakiwa wamecheza Mechi 1 pungufu.
Mapema Jana, Atletico Madrid, ikiwa kwao Vicente Calderon, ilitoka
0-0 na Sevilla waliocheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 61 baada ya Victor
Machin Perez Vitolo kulambwa Kadi za Njano 2 na kutolewa kwa Kadi
Nyekundu.
Huko Estadio Benito Villamarin hapo Jana, Real Madrid walinusurika
kichapo kutoka kwa Real Betis baada ya Karim Benzema kuwaokoa
aliposawazisha katika Dakika ya 71 na Mechi kwisha 1-1.
Real Betis, ambao hawajashinda katika Mechi zao 11 zilizopita, walifunga Bao lao Dakika ya 7 kupitia Alvaro Cejudo.
Kwenye Mechi hiyo, Cristiano Ronaldo, aliekuwa goigoi, alikosa Bao
kadhaa akiungana na James Rodriguez aliekosa nafasi 2 za wazi.
Sare hii imemfanya Kocha mpya wa Real, Zinedine Zidane, aendelee na
rekodi ya kutofungwa tangu atwae wadhifa huu mapema Mwezi huu kutoka
kwa Rafa Benitez aliefukuzwa.
Barca sasa wako kileleni wakiwa na Pointi 48 kwa Mechi 20 wakifuata
Atletico wenye Pointi 48 pia kwa Mechi 21, kisha Real Pointi 44 kwa
Mechi 21 na wa 4 ni Villareal wenye Pointi 41 kwa Mechi 21.
Hakuna maoni :