MENEJA
wa Arsenal Arsene Wenger amesema Timu yao kwa mara nyingine tena
wamekuwa waathirika wa Straika wa Chelsea Diego Costa aliesababisha
Senthafu wao Per Mertesacker adungwe Kadi Nyekundu katika Dakika ya 18
kwenye Mechi iliyochezwa Jumapili huko Emirates na Chelsea kuifunga
Arsenal 1-0.
Dakika 5 baada ya Mertesacker kutolewa nje, Diego Costa alifunga Bao pekee na la ushindi kwa Chelsea.
Wenger ameeleza: “Costa amesababisha Wachezaji wetu Wawili wapewe
Kadi Nyekundu katika Mechi zetu 2 zilizopita. Je ni uamuzi sahihi au
hapana? Sijui. Huo ni ukweli bila kumtuhumu chochote!”
Mwezi Septemba Mwaka Jana, Costa alikwaruzana na Sentahafu wa
Arsenal Gabriel ambae alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa tukio hilo na
Chelsea kuibuka kidedea kwa kuifunga Arsenal 2-0.
Msimu huu, Arsenal wamezoa Kadi Nyekundu 3 na zote ni za kwenye
Mechi dhidi ya Chelsea baada ya pia Santi Cazorla kutolewa nje katika
Mechi hiyo hiyo aliyotolewa Gabriel huko Stamford Bridge.
Arsenal wamezoa Kadi Nyekundu 7 kwenye Mechi na Chelsea na hizo ni
nyingi kupitana kwenye mapambano yao na Timu nyingine yeyote kwenye Ligi
Kuu England.
Akielezea tukio la Jana la Mertesacker kumwangusha Costa akiwa Mtu
wa mwisho huku Costa akielekea Golini, Wenger amesema hajui kama Costa
alikuwa Ofsaidi au Mertesacker alimgusa na kumwangusha Costa.
Wenger amesema: “Refa alikuwa mwepesi kutoa Kadi Nyekundu. Lakini tulilikabili tukio hilo vizuri na tulistahili Sare.”
Alipohojiwa kama Costa alitengeneza tukio hilo, Wenger alijibu:
“Ndio. Hiyo ndio Gemu ya Straika. Diego Costa ni mzuri kwa hayo!”
Lakini Bosi wa Chelsea, Guus Hiddink, hakukubaliana na amesema:
"Kulikuwa hamna wasiwasi. Ni pasi safi na Costa angeweza kwenda moja kwa
moja kumkabili Kipa Petr Cech lakini aliangushwa. Hilo ni wazi!”
Hakuna maoni :