Kocha
Herve Renard wa Ivory Coast ameteuliwa kuwa Kocha Bora barani Afrika.
Kocha huyo ameshinda tuzo hiyo katika tamasha la kuwatuza wachezaji bora
wa Afrikazilizofanyika jana jijini Abuja, Nigeria.
Renard
raia wa Ufaransa ameteuliwa kuwa kocha bora kutokana na mafanikio yake
kwa mwaka 2015. Mpinzani mkubwa kwake alionekana ni Patrice Carteron,
hata hivyo hakufua dafu.
Kocha
huyo ameiwezesha Ivory Coast kubeba ubingwa wa Afrika ikiwa ni mara yake
ya pili kufanya hivyo baada ya miaka michache kuwa ameiwezesha Zambia
kubeba ubingwa wa Afrika.
Lakini
Novemba 11, mwaka jana kocha huyo alitimuliwa kazi Lille ya Ufaransa
baada ya kuingoza timu hiyo kucheza mechi 13, ikaambulia pointi 13 tu.
Hakuna maoni :