Kikosi cha TP Mazembe kimeteuliwa kuwa kikosi bora barani Afrika mwaka 2015 katika tuzo za Mwanasoka Bora Afrika zilizofanyika jijini Abuja nchini Nigeria jana.
Mazembe ambao ni mabingwa watetezi barani Afrika, wametwaa tuzo hiyo na kuwapiga bao USM Alger ya Algeria ambao waliwafunga katika mechi zote mbili za fainali ubingwa wa Afrika.
Watanzania wawili, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanakipiga katika klabu hiyo ya Lubumbashi, DR Congo.
Katika mechi mbili za fainali, TP Mazembe ilianza kushinda ugenini kwa mabao 2-1, ikarejea nyumbani Lubumbashi na kushinda kwa mabao 2-0.
Katika mechi zote mbili, Mtanzania Samatta alifunga hivyo kuweka rekodi ya kufunga mabao mawili katika mechi mbili za fainali.
Pia katika mechi hizo mbili za fainali, Watanzania hao, Samatta na Ulimwengu, wote walicheza mechi zote mbili, hivyo mchango wao kwa Mazembe kuwa kikosi bora Afrika ni mkubwa sana.
Hakuna maoni :