Madereva wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam wamesema
watagoma kuendesha magari hayo kufuatia uongozi wa mabasi hayo kuwapa
mkataba wa kazi usiokidhi mahitaji.
Baadhi ya mahitaji hayo ni mshahara mdogo wa shilingi laki 4 kwa mwezi tofauti na makubaliano ya awali ya shilingi laki 8.
Wakiongea na Eatv leo, madereva hao wamesema pia wameshangazwa na
kitendo cha uongozi wa mabasi hayo kuwapa mkataba wa kazi bila ya
kuwapatia nakala yake jambo ambalo wamesema ni kinyume cha taratibu za
ajira.
Madereva hao ambao leo walikusanyika katika kituo kikuu cha mabasi
yaendayo haraka kilichopo eneo la Kamata wamesema tayari
walishatangaziwa malipo halisi kuwa ni shilingi laki 8 hivyo kitendo cha
kusainishwa mkataba wa malipo ya shilingi laki 4 hawakubaliani nacho.
Hakuna maoni :