Jeshi la Polisi Jumatatu hii limezima ghasia za wananchi
wenye hasira maeneo ya Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam baada ya
kupinga zoezi la bomoa bomoa kwa mara ya pili kufuatia kukataa kuondoka
katika eneo hilo kwa madai hawana pa kwenda.
Bi Fatuma akizungumza kwa uchungu
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii mmoja kati ya waathirika
wa bomoa bomoa hiyo, Bi Fatuma Said, amesema wanashindwa kuondoka
katika eneo hilo kwa kuwa hawana sehemu ya kwenda huku akiitaka serikali
kuwafikiria.
“Sio kwamba tumegoma kuondoka wengine sisi hatuna sehemu ya
kwenda,” alisema. “Sisi baada ya kubomolewa nyumba yetu tukashindwa
kuondoka kwa kukosa pa kwenda.Tukaamua kujenga hapa vijibanda ili
serikali itufikirie lakini tunashangaa leo asubuhi vibanda vyetu
vimewekwa X kwamba wanataka kubomoa. Saa tano tumeingiliwa kwenye
vibanda vyetu sisi tukakimbia wao wakachoma ndio baadhi ya wanacnhi
wakaingiwa na hasira na kwenda kuchoma matairi barabarani,”alieleza.
Hata hivyo Bongo5 ilijaribu kuzungumza na afisa wa polisi
aliyekuwepo katika eneo hilo, lakini alisema watatoa taarifa rasmi
kuhusu tukio hilo. Hadi sasa polisi wanawashikilia vijana kadhaa
wanaohusishwa na tukio hilo.
Tazama picha zaidi:
Hakuna maoni :