SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / POULSEN AELEZA KUHUSIANA NA SUALA LA UKOCHA SIMBA.


Aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars, Mdenishi, Kim Poulsen, amefunguka kuwa yupo tayari kuchukua mikoba ya Muingereza, Dylan Kerr ya kuifundisha Simba endapo viongozi wa klabu hiyo watamfuata na kuzungumza naye juu ya dili hilo.

Hivi karibuni Simba ilifikia uamuzi wa kuachana na Kerr baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo mbaya katika Ligi Kuu Bara pia kufanya vibaya kwenye Kombe la Mapinduzi.

Poulsen ambaye amekuja nchini kwa ajili ya mapumziko, tangu awasili wiki iliyopita amekuwa akienda uwanjani kuangalia mechi mbalimbali za ligi kuu huku akionekana kuwa makini na ‘kunoti’ baadhi ya matukio ya uwanjani.

Kocha huyo mwenye miaka 56, aliwahi kufundisha timu za vijana za Tanzania kuanzia mwaka 2011 mpaka 2012, kabla ya kukabidhiwa mikoba ya kuinoa Taifa Stars mwaka 2012 mpaka 2014.


Awali Simba ilikuwa ikimuhitaji kocha huyo aweze kuifundisha timu yao baada ya kuachana na Mserbia Goran Kopunovic, msimu uliopita, lakini mambo hayakuenda vizuri na kumpa Kerr jukumu hilo.

Akizungumzia ishu ya kuinoa Simba, Poulsen alisema wakati anaondoka Tanzania mwaka 2014, alitamani siku moja arudi nchini kama kocha na sasa amepata nafasi ya kuja kwa ajili ya mapumziko, hivyo hatakataa kama akifuatwa na viongozi wa Simba na kutakiwa kupewa mikoba ya kuinoa timu hiyo iliyoachana na Kerr wiki moja iliyopita.

“Kwa nini nikatae, nipo tayari kwa hilo kwani wakati naondoka hapa nchini baada ya kuachana na Stars nilitamani kurudi tena nikiwa kocha.

“Nimekaa Tanzania kwa miaka mitatu, hivyo nataka kufundisha tena hapa nchini, japo kwa sasa nimekuja kwa ajili ya mapumziko na mwishoni mwa mwezi huu natarajia kurudi nyumbani Denmark kuendelea na shughuli zangu, lakini nimekuwa nikienda uwanjani kuangalia baadhi ya mechi za ligi.

“Katika mechi nilizozishuhudia mpaka sasa, nimeziona Simba, Yanga na Azam zikicheza lakini siwezi kuongelea chochote juu ya ‘pafomansi’ zao kwani ni mapema mno, nahitaji kuziona zaidi na zaidi.


“Kesho (leo) kuna mechi za ligi tena, Simba itakuwa nyumbani (Uwanja wa Taifa, Dar) na Azam ugenini (Mkwakwani, Tanga), nitaenda kuiangalia Simba ikicheza lakini pia Yanga itakapocheza (kesho Alhamisi katika Uwanja wa Taifa) nitaenda pia,” alisema Poulsen.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply