Mchezaji Mbwana Samatta aliyejishindia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika
kwa wachezaji wa Ndani nchini Nigeria amezawadiwa na serikali kiwanja
kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam na fedha taslimu ambazo kiasi
chake hakijafahamika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mh.Lukuvi anayeonekana katika picha katika hafla iliyofanyika
kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na
viongozi kadhaa wa serikali.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika hafla hiyo ni
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye na Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi wengine
wengi wa serikali na wanamichezo.
Hakuna maoni :