SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / SHEIKH SALMAN ATEMBELEA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO, VPL MZUNGUKO WA 15 KUENDELEA KESHO.


PATA TAARIFA KAMILI:
SHEIKH SALMAN ATEMBELEA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO

VPL-SIT-LOGORais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Asia (AFC), na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa leo ametembelea wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, ambapo alifanya mazungmzo mafupi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel.


Katika mazugmzo hayo, Sheikh Salman ameielezea Serikali ya Tanzania nia ya FIFA kuendelea  kushirikiana na Serikali na TFF katika kuendeleza programu mbalibali za maendeleo ya mpira hasa wa vijana na wanawake.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Elisante  ameihakikishia FIFA kuwa nia ya Serikali ni kuona mpira unakua nchini na Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa TFF na FIFA ili kufikia azama hiyo.

Aidha pia ametoa wito kwa AFC kusaidiana na TFF katika masuala ya exchange programmes ili vijana wetu wapate uzoefu wa nje.
Sheikh Salman na ujumbe wake walitembelea ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) wakiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambapo walikutana na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanya na shirikisho, ikiwemo uwanja wa Karume, na Hostel zilizopo Karume.

Kiongozi huyo wa AFC, aliwasali nchini jana mchana kwa matembezi ya siku mbili chini ya mwenyeji wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi na anatarajiwa kuondoka nchini kesho.

VPL MZUNGUKO WA 15 KUENDELEA KESHO

Ligi Kuu ya Vodacom mzunguko wa 15 unatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo mitano, na Alhamisi kwa michezo mitatu kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu katika mzunguko huo. 

 
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Maafande wa JKT Ruvu watawakaribisha Simba SC, Ndanda FC watakua wenyeji wa Mbeya City kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.


Tanzania Prisons watakua wenyeji wa Coastal Union katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Stand United watacheza dhidi ya Toto Africans kwenye uwanja wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwakaribisha Azam FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Alhamisi ligi hiyo itaendelea kwa michezo mitatu, Mwadui FC watawakaribisha Kagera Sugar katika uwanja wa Mwadui, African Sports watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar uwanja wa Mkwakwani jijini Tnaga, huku Young Africans wakiwakaribisha Majimaji FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
IMETOLEWA NA TFF

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply