Manejimenti ya sahara media group ambao ni wamiliki wa Star Tv, RFA naKiss Fm imesema haijapata barua au taarifa rasmi yeyote kutoka mamlaka ya mawasilano Tanzania TCRA ya kutakiwa kufunga vyombo vyake.
Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba
wamekuwa wakilipia leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi
ya shilingi milioni 500 hadi kufikia mwezi October 2015.
Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya
TCRA kanda ya Mwanza, makao makuu na sahara media group limited
nakukubaliana juu ya utaratibu wa malipo ya ada husika.
Lakini menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA
kutangaza kuvifungia vituo vyake kupitia mkutano wa vyombo vya habari
bila kujali athari zakufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa
huduma.
Sahara media group limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa
ada kwa dola za kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo
kila mara na kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama.
Menejimenti pia imelaani taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa
wiki nakuvipa vituo husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua
dhahiri jumamosi na jumapili sio siku za kazi.
Menejimenti ya star tv inawaondoa wasiwasi watazamaji na
wasikilizaji wake, hatua thabiti zitachukuliwa ili kumaliza tatizo
hili kwa sahara media group limited na TCRA Kwa Kufuata Misingi Ya
Sheria, Kanuni Na Maridhiano.
Hakuna maoni :