Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi ameviomba radhi vilabu vya
ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kutokana na timu ya Azam kupewa ruhusa
na TFF kwenda nchini Zambia kushiriki mechi za kirafiki ambazo hazipo
kwenye kalenda ya CAF, FIFA wala chama chochote cha soka kati ya
Tanzania na Zambia.
Malinzi amekiri makosa yamefanyika ndani ya TFF kuiruhusu
Azam lakini amejitetea kwamba wakati ruhusa hiyo inatolewa yeye hakuwepo
nchini.
Malinzi pia amesema Yanga kutofanya uchaguzi mkuu wa
viongozi wa klabu yao haimaanishi kwamba wako juu ya sheria na amewataka
Yanga kuheshimu katiba yao pamoja na ile ya TFF.
“Naomba nivitake radhi vilabu vyote 15 vinavyoshirili ligi
kuu Tanzania bara kwa kosa lililofanyika la kuwaruhusu Azam FC kwenda
Zambia kucheza mechi za kirafiki, najua maamuzi yamefanyika mimi nikiwa
Burundi, lakini kama kiongozi nakiri kosa kufanyika na naviomba radhi
vilabu vyote”.
“Kuhusu Yanga kutofanya uchaguzi ukweli ni kwamba, Yanga hawapo juu ya sheria na wanapaswa kuheshimu katiba yao na ya TFF”.
Kuondoka kwa Azam kunasababisha mechi zinazoihusu timu hiyo
kusogezwa mbele na kusababisha viporo vya mechi visivyokuwa vya lazima
na kuvisababishi gharama na usumbufu vilabu ambavyo vingecheza na Azam
mechi hizo.
Malinzi pia ametuma salu za rambirambi kwa familia, ndugu
jamaa na marafiki wa Epaphra Swa aliyefariki jana asubuhi kwenye
hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Epaphra Swai alikuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na Mwenyekiti wa Chama cha
Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu.
Hakuna maoni :