• Manchester City (4-2-3-1): Hart 7, Maffeo 6.5, Stones 7 (Adarabioyo 60, 6)...

  • SALVATORY EDWARD Kiungo wa zamani wa timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kide...

  • Baada ya kikosi cha Mwadui FC kuchapwa kwa bao 1-0 katika mechi yao ya Lig...

  • Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka bayana kuwa, lipo kwenye mpango wa ...

SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Updates Kuhusu Kujiuzulu Kwa Kamati ya Miss Tanzania Leo.

Miss Tanzania
Kama ya shindano la Miss Tanzania, imetangaza kujiuzulu.
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Ijumaa hii, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya maandilizi ya shindano hilo Juma Pinto, amedai kuwa sababu ya kujitoa kwenye kamati hiyo ni kutokana na kushindwa kujua nini majukumu yao na yale ya kampuni inayoyaanda, Lino Agency.

Amedai kuwa awali iliwekwa wazi kuwa ni kamati hiyo ndiyo itakayoratibu mashindano hayo huku Lino Agency ikibaki kuwa washauri.

Pinto amesema Lino imeendelea kufanya kazi yake lakini wao wakibaki bila kujua kinachoendelea. “Sisi tumeona tuje tuzungumze tu kwamba sisi hatupo huko,” amesema Pinto.

Naye msemaji wa kamati hiyo, Jokate Mwegelo amesema kutokana na ukubwa wa kile Miss Tanzania imefanya kwa wasichana, wasilichukulie kwa wepesi na kiubinafsi.

“Waangalie wasichana wa Tanzania wanawatoaje? Na kuwatoa ni kuhakikisha kwanza misingi ya shindano lenyewe iwe ya kueleweka. Kama misingi haieleweki ndio tunarudi kule kule,” amesema Jokate.

Aliongeza kuwa makosa yaliyojitokeza miaka iliyopita pamoja na malalamiko mengi dhidi ya shindano hilo yanapaswa kufanyiwa kazi.

Kamati hiyo ya Miss Tanzania ilitambulishwa August mwaka ikiwa na wajumbe wafuatao:

1.Juma Pinto – Mwenyekiti
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi – Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe

Wajumbe wa Sekretariet ni:

1. Dr.Ramesh Shah
2. Hidan Ricco
3. Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni

«
Next
JUMAMOSI, LEICESTER AU CITY, NANI KUONGOZA, MAN UNITED OLD TRAFFORD NA ‘WATAKATIFU.
»
Previous
Breaking News;Uchaguzi wa Marudio Zanzibar Kufanyika Mwezi Machi 2016.

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply