LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumamosi 23 Januari 2016
1545 Norwich v Liverpool
[Mechi kuanza Saa 12 Jioni]
Crystal Palace v Tottenham
Leicester v Stoke
Man United v Southampton
Sunderland v Bournemouth
Watford v Newcastle
West Brom v Aston Villa
2030 West Ham v Man City


Katika Mechi za Saa 12 Jioni, Manchester United, ambao wameanza vyema 2016 baada ya kulegalega Mwezi Desemba, wako kwao Old Trafford kucheza na Southampton ambayo waliifunga 3-2 katika Mechi ya kwanza Msimu huu huko Saint Mary’s Park.
Vinara wa Ligi, Leicester City, ambao wamefungana kwa Pointi kileleni na Arsenal, wako kwao King Power Stadium kucheza na Stoke City kwenye ambayo inaweza kuwafanya watwae uongozi wa Ligi hasa kwa vile Arsenal wanacheza Jumapili na Chelsea huko Emirates.
Lakini, Leicester wakiteleza, baadae Usiku wa Jumamosi Man City, wakiifunga West Ham huko Upton Park, wanaweza kuongoza Ligi Kuu England.
Jumapili 24 Januari 2016
1630 Everton v Swansea
1900 Arsenal v Chelsea
Hakuna maoni :