SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / VPL: MABINGWA YANGA MOTO, YAFUMUA 5, TAMBWE BALAA, APIGA HETITRIKI, WARUDI KILELENI.





LIGI KUU VODACOM
Matokeo:
Alhamisi Januari 21
Mwadui FC 2 Kagera Sugar 1
African Sports 0 Mtibwa Sugar 0
Yanga 5 Majimaji 0

VPL-SIT-LOGOLigi Kuu Vodacom, VPL, iliendelea Leo na Mabingwa Watetezi Yanga kuitandika Majimaji FC 5-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kurudi tena kwenye Kiti chao cha uongozi wa VPL-JAN21Ligi huku Straika wao Amisi Tambwe akipiga Hetitriki.

Yanga walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 4 kupitia Thaban Kamusoko na Bao hilo kudumu hadi Mapumziko.

Bao la Pili la Yanga lilifungwa Dakika ya 47 na Donald Dombo Ngoma baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Thaban Kamusoko.

Katika Dakika ya 57 Amisi Tambwe aliipa Yanga Bao la 3 na hilo ni Bao lake la 11 kwenye VPL likimfanya azidi kupaa juu kileleni katika Safu ya Mfungaji Bora.

Tambwe tena akaipa Yanga Bao la 4, likiwa Bao lake la 12 kwenye VPL, katika Dakika ya 72 baada ya muvu murua ya Timu ya Yanga.

Yanga walifunga Bao lao la 5 Dakika ya 88 Mfungaji akiwa tena Tambwe akipiga Bao hilo, likiwa lake la 13 kwa VPL, na ni Hetitriki kwa Mechi hii.
Hadi mwisho Yanga 5 Majimaji FC 0.

Ushindi huu umewapa Yanga uongozi wa VPL wakiwa na Pointi 39 kwa Mechi 15 sawa na Azam FC lakini wao wako juu kwa ubora wa Magoli.

LIGI KUU VODACOM
Ratiba:
Jumamosi Januari 22
Coastal Union v Yanga
Simba v African Sports
JKT Ruvu v Majimaji
Tanzania Prisons v Azam FC 
Mtibwa Sugar v Stand United
Mwadui FC v Toto Africans

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply