SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Rais Magufuli Amemsimamisha Kazi Kamishna wa Uhamiaji Kupisha Tuhuma zinazomkabili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Bwana Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Utawala na fedha Bwana Piniel Mgonja ili kupisha uchunguzi, kufuatia dosari alizozibaini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Charles Kitwanga alipotembelea Idara ya Uhamiaji hivi karibuni.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amezitaja dosari hizo kuwa ni pamoja na tuhuma za rushwa, ukusanyaji mbaya wa maduhuli ya serikali, ukiukwaji wa taratibu za manunuzi na utendaji mbovu.

Balozi Sefue amesema watendaji hao wakuu wa Uhamiaji wamesimamishwa kazi mara moja hadi hapo uchunguzi utakapokamilika na kwamba endapo watabainika kutokuwa na makosa Rais ataamua hatma yao.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply