MHARIRI wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Mhariri wa gazeti la
MwanaHALISI ambaye pia ni mwandishi Mwandamizi wa gazeti la Mawio, Jabir
Idrissa jana wameachia kwa dhamana na Jeshi la Polisi, baada ya
kutimiza masharti ya dhamana hiyo.
Wahariri hao walijisalimisha juzi majira ya saa tisa jioni baada ya
kupokea taarifa ya kutafutwa na jeshi la polisi kwa siku tatu na
kuhojiwa kwa masaa nane, lakini walipomaliza majira ya saa tano usiku
walinyimwa dhamana na polisi kwa madai jana asubuhi wangepelekwa
mahakamani.
Jeshi la polisi walishindwa kuwapeleka mahakamani wahariri hao, lakini
walifungua dhamana kwa masharti ya kila mtuhumiwa kuwekewa dhamana ya
Sh. 20 milioni, huku akitakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili.
Mkina na Jabir wametimiza masharti hayo kwa kudhaminiwa na wadhamini
wawili kwa kila mmoja huku kila mdhamini akisaidi bondi ya Sh. 10
milioni.
Wahariri hao wametakiwa kuripoti kituoni hapo kila siku saa mbili asubuhi mpaka hapo watakapopewa utaratibu mwingine.
Udaku Special Blog
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :