Mshambuliaji
Mganda, Hamisi Kiiza ameonyesha kweli ni mtambo wa mabao baada ya
kufunga bao la 10 na kumfikia mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga.
Kiiza
raia wa Uganda amefunga bao moja wakati akiiwezesha kuitwanga JKT Ruvu
kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar, leo.
Bao
la pili la Simba lilifungwa na Dani Lyanga lakini Kiiza akaanza kwa
kufunga bao lake la kumi kwa mkwaju wa penalti na kumfikia Kiiza raia wa
Burundi aliyekuwa anaongoza kwa mabao 10.
Mechi
iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar, Kiiza alifunga bao pekee katika
ushindi wa 1-0 na kumvuka Donald Ngoma raia wa Zimbabwe mwenye mabao
nane lakini akawa amemfikia Elias Maguri mwenye mabao tisa na leo
amefunga tena moja na kumfikia Tambwe.
Kiiza
ndiye alianza kwa kasi juhudi za ufungaji, baadaye akaanza kusumbuliwa
na majeraha, hali iliyompa Tambwe nafasi ya kumpita kwa idadi ya mabao
kabla ya yeye kufunga mabao mawili katika mechi mbili.
Hakuna maoni :