Pamoja
na kuanza kwa kufunga mabao mawili, Bayern Munich imeshindwa kuyalinda
baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 ikiwa ugenini dhidi ya Juventus
ya Italia.
Mechi
hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa tamu na ya kuvutia, Bayern
ilipata mabao yake kupitia Thomas Muller katika dakika ya 43 na Arjen
Robben akafunga la pili katika dakika ya 55.
Lakini
wenyeji Juventus wakaendelea kuonyesha ni wabishi walipopata bao katika
dakika ya 63 kupitia Paul Dyabala kabla ya Stefano Sturaro kusawazisha
katika dakika ya 76.
Majibu ya nani anasonga hadi robo fainali, yatapatikana katika mechi ya pili jijini Munich, Ujerumani.
Hakuna maoni :