Wengi
waliamini Arsenal haina ubavu wa kuizuia Barcelona katika mechi hiyo ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, leo.
Kweli wamepatia, kwani Arsenal imelazwa kwa mabao 2-0 huku ikihenyeshwa kwa kiasi kikubwa uwanjani.
Lionel
Messi ndiye alifunga mabao hayo mawili katika kipindi cha pili, akianza
na lile la kwanza katika dakika ya 71 baada ya kupokea pasi safi ya
Neymar aliyeambaa pembeni mwa uwanja kwa kasi.
Messi
tena, aliangushwa na mwamuzi Cuneyt Cakir kutoka Uturuki, akaamuru
ipigwe penalti. Messi hakufanya ajizi, akaikwamisha wavuni katika dakika
ya 84.
Dakika tatu baadaye, kipa Petr Cezch wa Arsenal akafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kichwa wa Neymar.
Katika
kipindi cha kwanza, Arsenal walipoteza nafasi tatu za kufunga ambazo
zinegeweza kubadilisha mambo. Hata hivyo wachezaji wake walionekana kama
ni wenye hofu na walioshindwa kufanya mambo kwa uhakika.
Kama wangekuwa watulivu, huenda wangepusha kunyanyaswa muda mrefu na Barcelona walioonekana kama wako nyumbani.
Hakuna maoni :