Beki
wa Simba, Abdi Banda jana, amejiondoa katika kikosi cha Simba
kinachotarajia kuivaa Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Banda
amesema ameumia na atakaa nje ya uwanja kwa miezi miwili huku akijipa
matumaini, lakini Simba wakaonekana kutotaka kulizungumzia suala hilo.
Banda
ambaye ana uwezo wa kucheza hadi namba nne tofauti uwanjani,
alithibitisha kupata majeraha yake ya misuli kupitia Ukurasa wa Kijamii
wa Facebook aliyeandika ujumbe uliosomeka hivi: “Dah nitamis sana kurudi
uwanjani, miezi miwili ni mingi sana, dah ila ntapona.”
Ujumbe wa beki huyo, uliendana na picha yake aliyoiweka akiwa amelala kitandani hospitalini akifanyiwa vipimo.
Daktari
wa Simba wala viongozi, hakuna aliyekuwa tayari kulizungumzia suala
hilo, kwani baada ya muda fulani, Banda alifuta ile post yake kwenye
Facebook.


Hakuna maoni :