SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / UEFA CHAMPIONZ LIGI: JUMATANO NI ROMA V REAL, GENT V WOLFSBURG.

UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
JUMATANO 17 FEB 2016
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
KAA Gent v VfL Wolfsburg
AS Roma v Real Madrid

RONALDO-ALIZA-UCLMechi za kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, zimeanza Jumanne na Jumatano zipo tena Mechi nyingine 2.

IFUATAYO NI TATHMINI YA MECHI HIZI ZA JUMATANO:
AS Roma v Real Madrid
Ingawa AS Roma waliwahi kuwabwaga nje Real Madrid kwenye hatua hii ya UCLL Mwaka 2008, safari hii Wachambuzi wanawapa nafasi kubwa Vigogo hao wa Spain kusonga.

AS Roma, sasa wakiwa tena chini ya Kocha Luciano Spalletti, wapo kwenye mfululizo wa ushindi wa Mechi 4 lakini katika Miaka ya hivi karibuni wamekuwa dhaifu huko Ulaya wakikutana na Timu ngumu kiasi cha kuchapwa 6-1 na Barcelona na 7-1 na Bayern Munich katika Misimu Miwili iliyopita ya Mashindano haya.

Ingawa AS Roma wako kwao Stadio Olimpico Jijini Rome Nchini Italy, Real inatisha kwenye michuano hii baada ya kubandika Bao 19 Msimu huu kwenye UCL Bao ambazo hakuna Timu nyingine iliyofikia.

Real, sasa wakiwa chini ya Lejendari wa France Zinedine Zidane baada ya kutimuliwa Rafa Benitez hivi karibuni, watatinga bila ya Gareth Bale lakini yupo Cristiano Ronaldo ambae ndie aliibuka Mfungaji Bora wa hatua za Makundi za UCL Msimu huu akiwa na Bao 11 huku Karim Benzema akiwa ni moto.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
REAL: Navas – Carvajal, Marcelo, Ramos, Varane – Kovacis, Kroos, Modric – Ronaldo, James, Benzema.
AS ROMA: Szczęsny – Digne, Rudiger, Manolas, Florenzi – Pjanic, Keita – Mohamed Salah, Perotti, El Shaarawy – Edin Dzeko

REFA: Pavel Královec [Czech Republic]
ROMA-REAL-USO
KAA Gent v VfL Wolfsburg
Hii si Mechi ya mvuto katika jukwaa la Mashindano haya ya Ulaya lakini ni Mechi itakayokuwa na ushindani mkubwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Gent, Klabu ya Belgium, kucheza UCL na walishangaza kwenye hatua za Makundi waliposhinda Mechi zao zote 3 za mwisho na kutinga Raundi hii.

Gent, chini ya Kocha Hein Vanhaezebrouck, wanacheza na Wolfsburg ya Ujerumani ambayo imeshinda Mechi 1 tu ya Ugenini ya Bundesliga Msimu huu na sasa wapo Nafasi ya 8 wakiwa Pointi 26 nyuma ya Vinara Bayern Munich.
Udhaifu mwingine kwa Wolfsburg ni kumkosa Sentahafu wao Naldo ambae yuko Kifungoni na hili litawatia majaribuni Kipa Diego Benaglio na Kiungo Mkabaji Josuha Guilavogui
Kwa Wenyeji Gent, tegemezi kubwa kwao ni Straika wao Laurent Depoitre anaelishwa na Viungo Danijel Milicevic na Sven Kums.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

GENT: Sels; Asare, Mitrović, Nielsen; Kums, Neto; Dejaegere, Milicevic, Foket; Simon, Depoitre.
WOLFSBURG: Casteels; Träsch, Knoche, Dante, Rodriguez; Arnold, Gustavo; Vieirinha, Draxler, Schürrle; Kruse.

REFA: Svein Oddvar Moen [Norway]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa
JUMANNE 16 FEB 2016 

Benfica v Zenit Saint Petersburg
Paris St Germaine v Chelsea

JUMATANO 17 FEB 2016 

KAA Gent v VfL Wolfsburg
AS Roma v Real Madrid

JUMANNE 23 FEB 2016
Arsenal v Barcelona
Juventus v Bayern Munich

JUMATANO 24 FEB 2016
Dynamo Kiev v Man City
PSV Eindhoven v Atletico Madrid

Marudiano
JUMANNE 8 MAR 2016
Real Madrid v AS Roma
VfL Wolfsburg v KAA Gent

JUMATANO 9 MAR 2016
2000 Zenit St Petersburg v Benfica
Chelsea v Paris St Germaine

JUMANNE 15 MAR 2016
Atletico Madrid v PSV Eindhoven 
Man City v Dynamo Kiev 
  
JUMATANO 16 MAR 2016
Barcelona v Arsenal
Bayern Munich v Juventus 


TAREHE MUHIMU:
Raundi za Mtoano:
-Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16: Desemba 14
**Mechi Februari 16/17/23/24 na Marudiano Machi 8/9/15/16

-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13

-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply