JANA huko Stade Regional Nyamirambo Mjini Kigali Nchini Rwanda, kwenye Fainali ya CHAN 2016, ambazo ni Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wachezao ndani ya Afrika, Congo DR wameinyuka Mali 3-0 na kutwaa Ubingwa huu wa Afrika kwa mara ya pili.
Congo DR, walitwaa Kombe hili mara ya kwanza Mwaka 2009, na Leo waliongoza 1-0 hadi Haftaimu kwa Bao la Meschack ambae pia alifunga Bao lao la pili Kipindi cha Pili na Bolingi kupata la 3.
Katika Mechi ya awali hii JANA kusaka Mshindi wa 3, Ivory Coast iliifunga Guinea 2-1 kwa Bao za Mohammed Youla, aliejifunga mwenyewe Dakika ya 33 na Gbagnon Anicet Badie kupiga la pili Dakika ya 35 huku Guinea wakipata Bao lao Dakika ya 86 Mfungaji akiwa Alseny Bangoura.
ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 30
Rwanda 1 Congo DR 2 [Congo DR 2 Rwanda 1 baada ya Dakika za Nyongeza 30]
Cameroun 0 Ivory Coast 0 [Ivory Coast 3 Cameroun 0 baada ya Dakika za Nyongeza 30]
Jumapili Januari 31
Tunisia 1 Mali 2
Zambia 0 Guinea 0 [0-0 baada ya Dakika za Nyongeza 30, Guinea wasonga Penati 6-5]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 3
Congo DR 0 Guinea 0 [1-1 baada ya Dakika 120, Congo DR yashinda kwa Penati 5-4]
Alhamisi Februari 4
Mali 1 Ivory Coast 0
Jumapili Februari 7
Mshindi wa 3
Guinea 1 Ivory Coast 2
FAINALI
Congo DR 3 Mali 0
Hakuna maoni :