MABINGWA
Watetezi wa La Liga huko Spain, FC Barcelona, wameendelea kuongoza La
Liga wakiwa Pointi 3 mbele baada ya Jana kuifinga Levante 2-0.
Timu ya Pili ni Atletico Madrid ambao Jana waliichapa SD Eibar 3-1
na Real Madrid wako Pointi 1 nyuma yao baada Jana pia kushinda Ugenini
2-1 dhidi ya Granada.
Barca, walioanza mapema Mechi yao na Levante, walipata Bao zao
kupitia David Navarro aliejifunga mwenyewe na kisha Luis Suarez kupiga
la pili na hilo likiwa Bao lake la 38 Msimu huu.
Suarez anaongoza Ufungaji Bora wa La Liga akiwa na Bao 20
akifuatiwa na Wachezaji wawili wa Real, Cristiano Ronaldo na Karim
Benzema, wenye Mabao 19 kila mmoja.
Pia ushindi huo wa Barca, chini ya Kocha Luis Enrique, umewafanya
waikamate rekodi yao ya Msimu wa 2010/11 wakiwa chini ya Pep Guardiola
waliposhinda mfululizo Mechi 23 na Sare 5 bila kufungwa.
Kwenye Mechi ya Granada na Real, Bao za Real zilifungwa na Karim Benzema na Luka Modric.
Nao Valencia, chini ya Kocha Gary Neville, walifungwa 1-0 ugenini
na Real Betis na hii ni Mechi ya 12 ya La Liga tangu Mchezaji huyo wa
zamani wa Manchester United aiongoze Valencia bila ushindi kwenye Ligi
hiyo.
Hakuna maoni :