MABINGWA
Watetezi wa Kombe la Mfalme wa Spain ambalo huitwa Copa del Rey, FC
Barcelona, Jana walitoka Sare 1-1 na Valencia katika Mechi ya Pili ya
Nusu Fainali na kutinga Fainali kwa Jumla ya Mabao 8-1.
Katika Mechi ya kwanza Barca walinyuka Valencia 8-0.
Jana huko Mestalla, Valencia, walio chini ya Garry Neville,
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, walitangulia kufunga kwa Bao la
Alvaro Negredo lakini Barca, wakicheza bila ya Mastaa wao wengi
walisawazisha kwa Bao la Wilfrid Kaptoum alietokea Benchi.
Kwenye Fainali, Barca watacheza na Mshindi kati ya Celta Vigo na
Sevilla ambao wanarudiana Leo huku Sevilla wakiwa wameshinda 4-0 katika
Mechi ya kwanza.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Valencia
Domenech; Vezo, Santos, Diallo, Gaya; Danilo, Villalba, Zahibo; Mina, Negredo, Piatti
Barcelona:
Ter Stegen; Adriano, Bartra, Vermaelen, Mathieu; Rakitic, Samper, Sergi; Vidal, Munir, Sandro

Hakuna maoni :