Huku
ikiendelea kusubiri ishu yake kama ipande Ligi Kuu Bara au la, Geita
Gold imesonga hadi hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la
Shirikisho la Azam Sports HD baada ya kumaliza Toto African kwa bao 1-0.
Pamoja
na kelele nyingi za Toto African inayoshiriki Ligi Kuu Bara kupitia kwa
msemaji wake, Geita Gold inayofunidishwa na Selemani Matola ilifanikiwa
kuonyesha soka safi na la kuvutia.
Shukurani
nyingi zitamwendea Omary Hassan aliyefunga bao safi katika dakika ya 64
na kuwaduwaza Toto African waliokuwa na mashabiki wengi zaidi kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo.
Hakuna maoni :