Beki
wa Simba, Hassan Ramadhan Kessy, amegomea mkataba wa timu hiyo baada ya
ule wa awali kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu huku akiutaka uongozi
wa timu hiyo kumpa milioni 60 ndiyo akubali kuanguka saini.
Kessy
ambaye alisajiliwa Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akitokea
Mtibwa Sugar ambapo kumekuwa na vuta nikuvute baina yake na klabu yake
hiyo tangu atue katika timu hiyo, awali aligoma kucheza kutokana na
kutopewa nyumba na kutomaliziwa fedha za usajili.
Hata
hivyo, mchezaji huyo ameonekana kuendelea kuwatesa viongozi wa Simba
kutokana na kumhitaji mchezaji huyo huku akionyesha kuwa ni wa gharama
kubwa.
Chanzo
cha kuaminika kutoka Simba kimeeleza kuwa, Kessy amewataka viongozi wa
timu hiyo kumpa kiasi cha shilingi milioni 60 ili aweze kuanguka saini
ya kuendelea kuitumikia timu hiyo, jambo ambalo limewashinda viongozi.
Aidha,
inadaiwa kuwa dau hilo kubwa analolitaka mchezaji huyo linachangiwa na
tetesi kuwa klabu kubwa za Yanga na Azam FC kumnyemelea hivyo kuwapa
ugumu.
“Awali
viongozi wa Simba walimuita Kessy ili aweze kuanguka saini, akakataa,
hivyo kuleta mvutano na kutaka alipwe milioni 60, kiasi ambacho uongozi
hauna uwezo nacho kulingana na hali halisi ya klabu kwa sasa.
“Uongozi
unaendelea na mazungumzo na meneja wa Kessy, Athuman Tippo kuona
watafikia wapi kwani kiasi cha fedha kilichopo ni kidogo na iwapo
itashindikana basi tutaachana naye na kutafuta mbadala wake,” kilisema
chanzo hicho.
Simu
ya Kessy haikupatikana hewani kwa muda wote tangu juzi na jana hakuwepo
hata benchi katika kikosi kilichocheza Kombe la FA dhidi ya Singida
United.
Hakuna maoni :