SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / LEICESTER CITY – NJIA NYEUPE UBINGWA, ILA JUMAMOSI KUIVAA ARSENAL HUKO EMIRATES.

LEICESTER-CITY-KINGPOWERSTADIUMPENGINE sasa Wadau wa Soka la England sasa wameanza kukubali kuwa Leicester City wana nafasi kubwa kutwaa Ubingwa hasa baada ya kuzichapa Liverpool na Manchester City na kupaa kileleni mwa Ligi Kuu England Pointi 5 juu ya Timu ya Pili Tottenham Hotspurs.

Kitu kikuu ambacho kitawasaidia sana kutwaa Ubingwa ni kutokana na wao kuwa na Mechi za Ligi pekee tofauti na Wapinzani wao wengine ambao wanakabiliwa na Mashindano ya Makombe mengine kama vile FA CUP, CAPITAL ONE CUP, UEFA CHAMPIONZ LIGI na LEICESTER-VARDY-MAHREZ-OKAZAKIEUROPA LIGI.

Wakati wengine, wakati mwingine, wakicheza Mechi 2 au 3 kwa Wiki, Leicester wao watacheza Mechi 1 tu kwa Wiki.

Mbali ya hilo, staili ya uchezaji ya Leicester ni tofauti kabisa na Wapinzani wao wakubwa, Manchester City, Arsenal na Tottenham, ambao humiliki Mpira kwa Wastani wa Asilimia 55 kwa Mechi wakati Leicester ni Asilimia 44 huku silaha yao kubwa ikiwa staili ya kaunta-ataki
Tegemeza lao kubwa la mfumo wao huko, chini ya Meneja wao Claudio Ranieri, ni Wachezaji wawili hatari.

Sentafowadi wao Jamie Vardy ndie mashine yao ya Magoli Siku zote akiwa tayari kupokea Pasi ndefu toka nyuma na kuchanja mbuga kwenda Golini kufunga.  

Yupo Winga wao Riyad Mahrez, kutoka Algeria, ambae hucheza Kulia na kuingia ndani na kutia Pasi kwa Mguu wake hatari wa Kushoto na pia kuifungia Magoli.
Lakini pia wanae Okazaki ambae mara nyingi humsaidia Vardy katika mashambulizi akitokea kwenye Kiungo ambako pia Leicester huwatumia Danny Drinkwater na N'Golo Kante.

LEICESTER-ZOEZI
Kwenye Difensi, kama Masentahafu, wapo Wes Morgan na Robert Huth, ambao ni nadra sana kwao kupanda juu sawa na Mafulbeki wao, na hasa Marc Albrighton, ambao hujaa kati badala ya kushika nafasi kwenye Winga.

BPL-FEB7B
Mechi inayofuata kwa Leicester City ni Jumamosi Ugenini na Arsenal ambayo iko Nafasi ya 3 ikiwa Pointi 5 nyuma ya Vinara hao.
Katika Mechi ya kwanza huko King Power Stadium, Arsenal iliichapa Leicester Bao 5-2.

LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
Jumamosi 13 Februari 2016
1545 Sunderland v Man United             
[Mechi kuanza Saa 12 Jioni]
Arsenal v Leicester           
Bournemouth v Stoke                
Crystal Palace v Watford            
Everton v West Brom                 
Norwich v West Ham                  
Swansea v Southampton            
Chelsea v Newcastle         
Jumapili 14 Februari 2016
1630 Aston Villa v Liverpool                 
1900 Man City v Tottenham 

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply