Shirikisho
la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetoa ratiba ya kuwania kufuzu
kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17
(U-17) zitakazofanyika nchini Madagascar mwakani kwa timu ya Taifa ya
Tanzania (Serengeti Boys) kuanza na Shelisheli.
Katika ratiba hiyo iliyotolewa makao makuu ya CAF, Cairo Misri na
nakala yake kutumwa kwa TFF, Tanzania imepangwa kucheza mchezo wa kwanza
dhidi ya Shelisheli kati ya Juni 24,25,26 nchini na marudaino kuchezwa
Julai 01,02,03 nchini Shelisheli.
Mshindi kati ya mchezo huo namba 15 na16 atacheza dhdi ya timu ya
Taifa ya Afrika Kusini katika hatua inayofuata ya 16 bora, na kisha
baadae kupata timu 8 zitakazofuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika
nchini Madagascar mwakani.
Fainali za Kombe la Dunia (FIFA U17) kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika mwezi Septemba waka 2017 nchini India.

Hakuna maoni :