Louis van Gaal anaamini Manchester United ipo kwenye mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu England hasa baada ya kuonyesha Soka safi katika Mechi zao 2 zilizopita.
Msimu huu, Meneja Van Gaal amekuwa akisakamwa sana baada ya Timu yake kucheza Soka la ovyo na kutokuwa na mtiririko mzuri wa ushindi.
Lakini Van Gaal anaamini ikiwa Man United itaifunga Chelsea huko Stamford Bridge Jumapili itakuwa imerudi kwenye reli kugombea Ubingwa.
Man United wapo Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 5 nyuma ya Timu ya 4 Arsenal na Pointi 10 nyuma ya Vinara Leicester City.
Hivi sasa Man United imepoteza Mechi 1 tu kati ya 8 ilizocheza mwisho na baada ya kuichapa Derby County 3-1 kwenye FA CUP na kisha kuitwanga Stoke City 3-0 kwenye Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford Jumanne iliyopita, Timu inaelekea kupata mwelekeo mpya wa ushindi.
Akiongea na Wanahabari hii Leo, Van Gaal alisema: “Hatukuzi mambo ila nina hisia tutaifunga Chelsea ingawa hilo ni gumu kwa vile chini ya Guus Hiddink hawafungwi. Tukishinda, Ligi yetu inaanza!”
Aliongeza: “Siku zote nimesema ni Mechi za Crystal Palace na Arsenal pekee ambazo Timu hizo zilionekana bora kupita Manchester United, nyingine zote sisi tulikuwa juu!”
Man United watatinga kucheza na Chelsea, ambao wako Nafasi ya 13, bila ya Majeruhi Bastian Schweinsteiger, Ashley Young, Marcos Rojo, Luke Shaw na Antonio Valencia.
Tangu wamtimue Jose Mourinho Mwezi Desemba, Chelsea, chini ya Meneja wa muda Guus Hiddink, haijapoteza Mechi yeyote katika Mechi zao 8 na ilitoka 0-0 na Man United Uwanjani Old Trafford Desemba 28 katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu.
BPL:
Ratiba
Jumamosi 6 Februari 2016
1545 Man City v Leicester
[Mechi kuanza Saa 12 Jioni]
Aston Villa v Norwich
Liverpool v Sunderland
Newcastle v West Brom
Stoke v Everton
Swansea v Crystal Palace
Tottenham v Watford
Jumapili 7 Februari 2016
1630 Bournemouth v Arsenal
1900 Chelsea v Man United
Jumatatu 8 Februari 2016
2300 Southampton v West Ham
Hakuna maoni :