• Manchester City (4-2-3-1): Hart 7, Maffeo 6.5, Stones 7 (Adarabioyo 60, 6)...

  • SALVATORY EDWARD Kiungo wa zamani wa timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kide...

  • Baada ya kikosi cha Mwadui FC kuchapwa kwa bao 1-0 katika mechi yao ya Lig...

  • Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka bayana kuwa, lipo kwenye mpango wa ...

SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Maalim Seif Sharif Hamad Amshushia Tuhuma Nzito Jakaya Kikwete..Adai Yeye Ndio Amevuruga Uchaguzi wa Zanzibar.

Katibu Mkuu wa (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa madai mazito kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka jana yalipinduliwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha, baada ya kupata baraka za Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Alisema, saa chache kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kutangaza kufuta uchaguzi huo, kituo kikuu cha kutangazia matokeo kilichokuweko Hoteli ya Bwawani kilizingirwa na vikosi vya jeshi na polisi na kwamba kitendo hicho kuwa ni “Mapinduzi ya Kikatiba”.

“Aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati ule alikuwa Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete na ndiye aliyepeleka vikosi vile baada ya kuona chama chake kimeelekea kushindwa kwa upande wa Zanzibar,” alisema Maalim Seif na kuongeza;
“Dkt. Shein wala Balozi Seif (Seif Ali Idd) hawamiliki jeshi wala polisi, vile ni vikosi vya Dk. Kikwete wakati ule na hawezi kukwepa lawama ya kuingilia uchaguzi wa Zanzibar.”

Maalim Seif pia amewashutumu baadhi ya viongozi wakiwemo wa dini wanaojaribu kupotosha ukweli na kuunga mkono uamuzi batili wa kurejewa uchaguzi uliotangazwa na ZEC.


TOA MAONI YAKO.

«
Next
ZUNGU, NKAMIA, WABUNGE WENGINE WAJUMUIKA NA WACHEZAJI, MAKOCHA SIMBA WAKIWA NJIANI KWENDA SHINYANGA
»
Previous
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea Afunguka Mazito Kuhusu Suala la Uchaguzi Zanzibar..'Nchi yetu itafika Pabaya'.

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply