MALINZI AMPONGEZA KIKWETE!
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanznaia (TFF), Jamal Malinzi
amempongeza Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa kukubali uteuzi wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) na GAVI utakaomfanya
kuwa bingwa wa chanjo na balozi wa mradi wa Africa United Duniani.
“Familia ya mpira wa miguu inajua umuhimu wa chanjo na hasa katika
maendeleo ya vipaji na wanamichezo kwa ujumla na jinisi chanjo
inavyoweza kuwapa watoto siyo tu fursa ya maendeleo bali pia haki ya
kuishi” ilisema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Rais wa TFF, Jamal
Malinzi.
Katika barua hiyo, Malinzi ameelezea furaha ya TFF kuona kiongozi
wa Tanzania akiongoza mapambano ya kuokoa afya na uhai wa kizazi cha
sasa na kijacho katika Afrika na dunia kwa ujumla.
“TFF itaunga mkono juhudi zako ili kufanikisha malengo yaliyowekwa
na ushirika wa chanjo” ilimalizia barua hiyo ambayo nakala yake imetumwa
kwa Rais wa Caf, Issa Hayatou.
LIGI KUU MZUNGUKO WA 17 KUENDELEA KESHO
Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa 17 unatarajiwa kuendelea kesho
Jumatano kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali, huku kila
timu ikisaka pointi tatu muhimu kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Kesho Jumatano, Simba SC watakua wenyeji wa maafande wa Mgambo
Shooting kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, JKT Ruvu
watawakaribisha Mbeya City katika uwanja wa kumbukumu ya Karume Ilala,
huku Mtibwa Sugar wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa
Manungu – Turiani.
Jijini Mbeya, Tanzania Prisons watakua wenyeji wa vinara wa ligi
hiyo Young Africans katika uwanja wa Sokoine, Wana kimanumanu African
Sports watacheza dhidi ya Mwadui FC uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga,
huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakiwakaribisha Majimaji FC katika
uwanja wa Kamabarage mjini Shinyanga.
Alhamisi ligi hiyo itaendelea kwa kuchezwa mchezo mmoja tu, Wagosi
wa Kaya Coastal Union watawakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Michezo ya viporo ya Azam FC imepangiwa ratiba, mchezo dhidi ya
Tanzania Prisons utachezwa Februari 24 uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,
huku mchezo dhidi ya Stand United ukichezwa Machi 16 katika uwanja wa
Azam Complex.
IMETOLEWA NA TFF
Hakuna maoni :