MALINZI KUSAKAMWA NA WAZENJI-TFF YAJIBU HAINA VITA NA ZFA.
>> TFF YAIPONGEZA RUVU SHOOTING!!
>> MALINZI AMPONGEZA MAKUNGA!!
PATA TAARIFA KAMILI:
TFF HAINA VITA NA ZFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limesema hakuna vita kati ya Shirikisho na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) bali mawasiliano yanaendelea kati ya TFF na vyombo husika kuhakikisha ZFA ambaye ni mwanachama mshiriki wa CAF anaendesha shughuli zake kwa mujibu wa taratibu
Kanuni na taratibu za CAF ziko wazi kuhusu nani aongoze Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na anapatikana kwa utaratibu upi.
Kikubwa ni kuzuia ZFA isipate madhara ya kufungiwa na Chama Cha Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
TFF YAIPONGEZA RUVU SHOOTING
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake, Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Ruvu Shooting kwa kufanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.
Malinzi ametuma salamu hizo kwa Mwenyekiti wa klabu ya Ruvu Shooting, Col. Charles Mbuge, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji na kuwataka kujipanga kwa maandalizi ya nguvu msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Ruvu Shooting imekua timu ya kwanza kupanda ligi kuu msimu huu baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa na kufikisha alama 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutoka katika hilo la B.
Washindi wawili kutoka maundi ya A, na B wataungana na Ruvu Shooting kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao huku timu zote zikiwa zimebakiza michezo miwili miwili kabla ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza msimu huu.
MALINZI AMPONGEZA MAKUNGA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Theophil Makunga kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) mwishoni mwa wiki.
Katika salamu hizo, Malinzi amempongeza Makunga kwa nafasi hiyo aliochaguliwa na kusema imani waliyonayo wahariri wenzake juu ya utendaji wake wa kazi ndio kumepelekea wao kumchagua kuongoza jukwa hilo.
Aidha Malinzi amewapongeza Deodatus Balile aliyechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na Neville Meena aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa jukwaa hilo na kuahidi kuwa TFF itaendelea kushirikiana nao.
IMETOLEWA NA TFF
Tagged with: MICHEZO
Hakuna maoni :