![]() |
| MWESIGWA |
Taarifa
ni kuwa hali si shwari ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
inaonekana kama kuna utulivu lakini nyuma ya pazia kuna tetesi kuwa
wafanyakazi wa taasisi hiyo hawajalipwa mishahara kwa muda wa miezi
miwili mfululizo sasa.
Habari
kutoka ndani ya TFF ambayo inaongozwa na Jamal Malinzi ni kuwa
malimbikizo ya mishahara yalianza tangu Desemba, mwaka jana na hata
mshahara wa Novemba, mwaka jana walilipwa mwisho wa Januari, mwaka huu.
“Haieleweki
hapa, hakuna mishahara kwa miezi miwili mfululizo sasa, huo wa Novemba,
mwaka jana ndiyo umetoka mwisho wa mwezi wa Januari. Hatujajua
inakuwaje kwa kweli,” alisema mtoa taarifa huyo.
“Maisha
ni magumu, hakieleweki na jamaa naona wanapita tu hapa. Pia hakuna
maelezo ya kutosha au ufafanuzi ambao ungefanya watu wajue nini cha
kufanya,” kilieleza chanzo.
Alipotafutwa
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa ambaye baada ya kuelezwa juu ya
tuhuma hizo alionyesha kutokuwa tayari kulitolea ufafanuzi suala hilo.
“Hayo
ni masuala ya utawala, siwezi kuyatolea ufafanuzi. Mambo ya maslahi ni
baina ya mwajiri na mwajiriwa, sasa siwezi kuanza kuyazungumzia au
kuyatolea ufafanuzi wowote,” alisema Mwesigwa na kukata simu.
SOURCE: CHAMPIONI


Hakuna maoni :